Wawakilishi wa mawakibu za Diwaniyya wanatembelea watu walioambukizwa virusi vya Korona na kuwapa moya wa kuvuka salama katika mtihani huo

Maoni katika picha
Kundi la wawakilishi wa mawakibu za Diwaniyya chini ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu pamoja na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, limewatembelea wagonjwa wa Korona waliolazwa kwenye kituo cha karantini maalum kwa ajili yao, ili kuwapa moyo na matumaini ya kuvuka salama kwenye mtihani huo.

Kiongozi wa wawakilishi hao wa mawakibu bwana Ali Mahadi Raadhwi amesema kuwa: “Wawakilishi wetu na mawakibu wanazo fungamana nazo wamefanya shughuli mbalimbali tangu siku za kwanza lilipotangazwa janga hili la Korona, tumesimama pamoja na wahanga kwa kugawa chakula na kutoa misaada tofauti, pamoja na msaada wa kitabibu, na tukio hili ni sehemu ya kuendeleza mshikamano wetu kwao”.

Akaongeza kuwa: “Tumekuja kuwatembelea ili kuwapa moyo na matumaini kuwa uwezekano wa kupona ugonjwa wa Korona ni mkubwa, matumaini yana nafasi kubwa ya kupona maradhi, kutabasamu, kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuongea maneno ya matumaini ni siraha kubwa ya kupambana na ugonjwa, huongoza kinga ya mwili. Aidha tumewapa zawadi za kutabaruku na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambazo zimewaongezea matumaini ya kupona na kuwapa moyo zaidi”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho na mawakibu pamoja na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kilitangaza kufanya opresheni kubwa kupitia mawakibu zilizo chini yake na wawakilishi wao waliopo mikoani, ya kusaidia familia za watu walio athirika na janga hili, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusimama pamoja na familia hizo na kuzipa msaada.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: