Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetangaza kuahirisha shughuli maalum ya kubadilisha bendera na kuweka bendera nyeusi zinazo ashiria huzuni katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam 1442h

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya Jumatatu ya mwezi (20 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (10 Agosti 2020m) umetangaza kuahirisha shughuli ya kubadilisha bendera kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika usiku wa kwanza wa mwezi mtukufu wa Muharam mwaka wa 1442h, kutokana na hali ya afya ambayo Iraq inapitia kwa sasa, na kuheshimu maelekezo yaliyo tolewa na sekta zinazo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: