Kituo cha utamaduni wa familia kimetoa program ya mchezo wa Alkafeel wa kielektronik

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa program ya mchezo iitwayo (Baraaimul-Kafeel Il-ktroniyyah) kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka (6 – 11), mchezo huo utawajenga kiutamaduni na kielimu, kwani umri huo ndio msingi mkuu wa jamii.

Mkuu wa kituo ustadhat Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Program ya Baraaimul-Kafeel sehemu ya kwanza imetengenezwa na jopo la wataalamu, inamafundisho mazuri yanayo endana na vijana wenye umri uliotajwa, kuna mashundisho ya (Dini, Akhlaq, Malezi, Maandalizi, Elimu na Michezo) inasaidia wazazi kutumia vizuri faragha za watoto wao, na kuondoa upweke walionao katika kipindi hiki cha korona pamoja na kuwaepusha na kuangalia mambo yasiyokuwa na faida yaliyopo kwenye mitandao ya intanet”.

Akaongeza kuwa: “Program hiyo inalenga mambo yafuatayo:

  • 1- Kuimarisha mawasiliano kati ya familia (hususan mama) na mtoto, kwa hiyo inawalenga wakinamama pia.
  • 2- Kutoa elimu na kumshawishi mtoto kufuata mwenendo wa kiislamu pamoja na kuwafundisha sira ya Ahlulbait (a.s).

Masharti ya kushiriki:

  • 1- Umri wa mshiriki uwe kati ya miaka (6 – 11) wavulana na wasichana.
  • 2- Program itachukua wiki moja kuanzia tarehe (10) hadi (16) mwezi wa nane 2020.
  • 3- Program inahusisha utumaji wa kipande cha video ya mtoto anayeshiriki ya usomaji wa Ayatu Kursiyyu baada ya kuihifadhi, video hiyo iwe ya dakika moja au moja na nusu, mpiga picha ashike vizuri kamera sambamba na kuzingatia vazi la hijabu kwa watoto wa kike, video hiyo itumwe kupitia link iliyopo kwenye ujumbe atakao pokea baada ya kutuma taarifa zake.
  • 4- Washindi (25) wa kwanza watapewa zawadi.
  • 5- Kuna zawadi za watakao fanya vizuri na kukosa nafasi ya ushindi.
  • 6- Kushiriki kwenye program hiyo fungua link ifuatayo: https://forms.gle/DuELGb4ZCbT9N2Rg8".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: