Kifaa cha kupima kuta ni mafanikio makubwa na maendeleo ya kisasa

Maoni katika picha
Kifaa cha kupima uimara wa kuta ni moja ya vifaa muhimu vya kihandisi na kiujenzi, chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa majibu ya kina yanayo endana na jambo linalo kusudiwa katika upimaji, kifaa hicho kimetengenezwa na wataalam wetu wa maabara nacho ni kifaa bora zaidi hapa Iraq.

Maelezo kuhusu kifaa hicho yametolewa na kiongozi wa maabara Mhandisi Ammaar Adnani: “Kifaa cha kupima ukuta (TGN) ni kifaa pekee kilicho tengenezwa na wataalam wa maabara ya majengo, nacho ni kifaa cha kisasa zaidi hapa Iraq, kimetengenezwa kutokana na mahitaji ya kifaa cha aina hiyo katika Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na baadhi ya mashirika”.

Akabainisha kuwa: “Kifaa hiki kimetengenezwa hapa nchini kutokana na ukubwa wa gharama yake na tukaona upo uwezekano wa kukitengeneza, kimewekwa kila kitu kinacho hitajika baada ya kukamilisha usanifu wake”.

Akaendelea kusema: “Kifaa hicho kina mitambo mingi ya kisasa inayo fanya kazi kwa haraka na kwa umakini wa hali ya juu, kifaa hiki ni maalum kwa ujenzi wa Iraq, miongoni mwa kazi zinazo fanywa na kifaa hicho ni:

Kwanza: kupima uimara wa ukuta kwa kwenda juu.

Pili: kupima uwezekano wa kupasuka pembezoni mwa ukuta.

Tatu: kupima uimara wa nguzo.

Kumbuka kuwa upimaji wa kuta kihandisi ni moja ya miradi muhimu, umeanzishwa kutokana na kuongezeka kwa miradi ya ujenzi inayo fanywa na Ataba tukufu, hivyo ikalazimika kuwa na kifaa maalum cha kupimia kuta za majengo, ili kutimiza mahitaji ya sekta hiyo, pamoja na upande wa kipato kutokana na kifaa hicho, kufuatia shughuli za ujenzi zinazo shuhudiwa katika mji mtukufu wa Karbala, miongoni mwa kazi za kifaa hicho pia ni kusaidia miradi ya ujenzi katika mkoa huu mtakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: