Kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa kwenye mikoa tofauti

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) wanaendelea kupuliza dawa kwenye miji na mikoa tofauti hapa nchini, hivi karibuni wamepuliza dawa kwenye mkoa wa Basra na Diwaniyya.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Wawakilishi wetu katika mkoa wa Basra wanaendelea na kazi ya kupuliza dawa, hususan baada ya baadhi ya ofisi kuanza kazi, hasa zinazotoa huduma za kijamii, wamepuliza ofisi zinazo toa huduma ya umeme na kumbi za serikali baada ya kupokea maombi kutoka kwenye ofisi hizo.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika watumishi wa kikosi chetu katika mji wa Diwaniyya wamepuliza dawa kwenye vituo vya ukaguzi na njia zinazo ingia katika mji huo, pamoja na kituo cha lango la Diwaniyya katika mji wa Afaka unao unganisha barabara za (Basra, Ammaarah, Bagdad na Diwaniyyah), katika mpango wa kusaidia jeshi la serikali kupambana na janga la Korona”.

Kumbuka kuwa Kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na janga la Korona, kamati hiyo imefanya kazi ya kupuliza dawa sehemu mbalimbali hususan kwenye makazi ya watu ndani na nje ya mji wa Karbala, na imefanya kila iwezalo katika kupambana na janga la Korona, ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kuosha, kuvisha sanda na kuzika watu waliokufa kwa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: