Baada ya kumaliza hatua ya kwanza: kazi ya ujenzi wa kituo cha tano cha kuhudumia watu walio ambukizwa Korona katika mkoa wa Bagdad imeingia katika hatua zingine

Maoni katika picha
Kazi ya ujenzi wa kituo cha tano cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji mkuu wa Bagdad ipo katika hatua za mwisho, baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya ujenzi huo, hivi sasa ujenzi unaendelea katika hatua zingine, mafundi na wahandisi wanaotekeleza mradi huo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi kubwa inayo onyesha matunda yake siku baada ya siku.

Mhandisi mkazi wa mradi bwana Karaar Barihi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya mradi huu, yenye mita (1377) ikiwa na vyumba (56) vya wagonjwa, mradi umeingia katika hatua mbili zingine, hatua ya kwanza inakazi nyingi, miongoni mwa kazi hizo ni kupaka rangi ukuta wa ndani baada ya kumaliza kuujenga pamoja na kuendelea kujenga dari na kuweka ruva za chini, sambamba na kujenga vyoo na mfumo wa maji taka na maji safi, sambamba na kufunga mitambo ya kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi na kuweka mfumo wa tahadhari na zimamoto”.

Akaendelea kusema: “Sehemu ya tatu inaukubwa wa mita (1100) ikiwa na vyumba (19) imekamilika kwa zaidi ya asilimia %85, kazi inayo endelea sasa hivi ni kufunga mitambo ya kutoa hewa chafu na mitambo mingine, pamoja na kuweka milango na madirisha na kufunga nyaya za umeme na viyoyozi, pamoja na kapaka rangi”.

Akafafanua kuwa: Kazi zilizo baki ni:

  • - Kumaliza kupaka rangi upande wa nje ya jengo.
  • - Kuandaa bustani kwa kupanda miti ya msimu na mauwa.
  • - Kuweka marumaru sehemu ya mbele ya jengo kwa nje.

Kumbuka kuwa jengo la Alhayaat la tano ni miongoni mwa majengo makubwa yaliyojengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu au ambayo bado yanaendelea kujengwa kwenye mikoa tofauti, ambayo ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia sekta ya afya kupambana na virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: