Mawakibu za kutoa misaada katika mtaa wa Dujaili zinagawa vifurushi (350) vya chakula kila wiki

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misaada katika mtaa wa Dujaili kwenye mkoa wa Waasit, zilizo chini ya idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu zimetangaza kuwa zinaendelea kutoa msaada wa vifurushi (350) vya chakula kila wiki katika eneo la mtaa huo, chini ya ratiba maalum iliyo andaliwa kwenye opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia wahanga wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa mawakibu katika mtaa huo Ustadh Aadil Katwan amesema: “Misaada hiyo inatolewa chini ya kauli mbiu isemayo (Baki nyumbani kwako sisi tunakufuata), tunagawa chakula kwa familia zenye kipato kidogo chini ya utaratibu maalum, tunatarajia kufikia familia nyingi zaidi, tumeanza kugawa katikati ya kitongoji hadi pembezoni kabisa ya kitongoji hicho”.

Akaongeza kuwa: “Vifurushi vya chakula tunavyo gawa vinamboga za majani na nafaka, tunaamini chukula hicho kinasaidia kupunguza ugumu wa maisha walio nao”.

Akasisitiza kuwa: “Imethibitika kwa kila mtu kuwa mawakibu za kutoa msaada ndio tegemeo kubwa wakati wa shida za aina zote, na zinafanya kazi chini ya maelekezo ya Marjaa, zipo tayali kufanya kazi katika mazigira yote”.

Familia zilizo pewa misaada hiyo zimesifu namna Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani anavyo wajali, wameshukuru waandaaji wa program hii.

Tambua kuwa Marjaa Dini mkuu ailitoa wito kwa mawakibu za kutoa msaada zilizo simama imara kusaidia wapiganaji wakati wa vita dhidi ya Daesh, zijitokeze kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo ambao wameathirika na marufuku ya kutembea iliyo wekwa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kwenye miji mingi ya Iraq, ndipo Atabatu Abbasiyya tukufu ikaanzisha program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo na wahanga wa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: