Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kinaendelea kuratibu semina kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kuratibu semina kwa njia ya mtandao kuhusu faharasi za kisasa chini ya kanuni ya (RDA) mark/21, tayali kimesharatibu semina nyingi, semina ijayo itaendeshwa kupitia program ya (ZOOM Cloud Meetings).
Semina hiyo itafanywa siku ya Alkhamisi ya mwezi (30 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (20 Agosti 2020m) na itaendelea kwa muda wa siku mbili saa kumi na moja jioni katika siku ya kwanza na saa tano kamili asubuhi hadi saa saba Adhuhuri katika siku ya pili kwa nyakati za Bagdad, mtoa mada ni bwana Ahmad Muhammad, kituo kimetoa wito kwa watu wanaohusika na sekta ya faharasi kusajili majina yao.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Hasanaini Mussawi, amesema kuwa: “Faharasi inaumuhimu mkubwa kwenye maktaba za aina zote, ni njia ya kuratibu maarifa na kufikia kwenye taaluma tofauti, kutokana na umuhimu huo pamoja na uzowefu walionao watumishi wetu katika sekta hii, tumeamua kuendesha semina hizi kwa njia ya mtandao kwa sababu ya kuwepo tatizo la maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa mada zitakazo fundishwa katika semina hii ni namna ya kuandaa kitaalamu taarifa za taaluma na mpangilio wa faharasi kwa kutumia kanuni ya mark/21, pamoja na kuangazia namna ya kuainisha baina yake na vyanzo vya taaluma zingine, na kuandaa rekodi kibailojia pamoja na mambo mengine”.

Akamaliza kwa kusema: Tambua kuwa kuna vyeti vya ushiriki kwa watakao shiriki (vitatumwa kwenye baruapepe zilizo sajiliwa), zingatia utambulisho wako na neno la siri utakalo tumia kuingia kwenye kikao (Meeting).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: