Kukamilika kazi za sehemu ya tatu na ya mwisho katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tano cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kitengo cha majengo na uhandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, siku ya Jumatano mwezi (29 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (19 Agosti 2020m), mafundi wake wamekamilisha kazi za sehemu ya tatu na ya mwisho katika ujenzi wa kituo cha tano cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Bagdad, kinacho jengwa kwenye eneo la hospitali ya Ibun Qaf chini ya idara ya afya ya Raswaafah, ukamilifu huo unaungana na sehemu mbili zilizo kamilika siku za nyuma na sasa mradi umekamilika kwa asilimia %99, ujenzi huu unafanywa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (5000), jengo linavyumba vya wagonjwa (118), pamoja na zaidi ya vyumba ishirini vya madaktari, wauguzi na ofisi, kazi iliyo baki ni kuweka mabango elekezi na kufanya usafi kwa ajili ya maandalizi ya ufunguzi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Karaar Barihi aliyo toa kwa mtandao wa Alkafeel: “Sehemu ya tatu ilihusisha eneo lenye ukubwa wa mita (1100) ikiwa na vyumba (19), asilimia kubwa ni vyumba vya idara na vya wahudumu, vimejengwa kwa kufuata vigezo vilivyo wekwa na idara ya afya”.

Akafafanua kuwa: “Kazi inayo endelea hivi sasa ni kutengeneza bustani. Kazi hiyo inafanywa na shamba boy wa Alkafeel, na kusafisha baadhi ya maeneo ya jengo, kisha yatawekwa mabango elekezi mbalimbali halafu litakuwa tayali kwa ajili ya ufunguzi na kuanza kutoa huduma”.

Kumbuka kuwa kituo cha Alhayaat cha tano, ni miongoni mwa vituo vikubwa vinavyo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mikoa tofauti, vituo hivi ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia wizara ya afya hapa Iraq katika kupambana na janga la Korana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: