Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika uzinguzi wa kumbukumbu ya “Shekh muimbaji”.

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa kumbukumbu ya (Shekh muimbaji), katika wilaya wa Hindiyya (Towareji) ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Uwekaji wa kumbukumbu hiyo utadumisha juhudi za muimbaji wa Husseiniyya marehemu Shekh Jaasim Nawini, mtumishi wa mimbari ya Husseiniyya katika kizazi cha kwanza, aliitumikia mimbari katika nusu ya kwanza ya karne iliyopita, alifariki tarehe (5 Aprili 2020m).

Aliasisi shule ya kufundisha usomaji wa tenzi na mashairi ya Husseiniyya miaka (70) iliyopita, ameshiriki kutoa huduma kwa mara ya mwisho katika mwezi wa Muharam wa mwaka jana (1441h).

Hafla hiyo ilifuata kanuni zote za afya na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kaimu mkuu wa wilaya Ustadh Muntadhir Shafi na kundi la waimbaji na mashekhe watukufu, umesomwa muhtasari wa maisha ya marehemu na namna alivyo tumikia mimbari ya Husseiniyya, hafla hiyo ikapambwa na visomo vya kaswida zake.

Mwisho wa hafla wawakilishi wa Ataba mbili tukufu wakapewa midani kama ishara ya kupongeza juhudi zao za kuwahudumia watumishi wa mimbari ya Husseiniyya, aidha mfadhili wa uandaaji wa kumbukumbu hiyo akapewa midani pia, mambo yote yamefanywa na familia ya marehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: