Rais wa mtandao wa habari Al-Iraaqiyyu amesema kuwa: Miradi ya Atabatu Abbasiyya ni ya pekee na bidhaa zake zinachuana kwa ubora na bidhaa za kigeni

Maoni katika picha
Rais wa mtandao wa habari Al-Iraaqiyyu Dokta Nabiil Jaasim amesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya ni ya pekee, na bidhaa zake zinachuana kwa ubora na bidhaa za kigeni. Amesema hivyo baada ya kutembelea miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Alkhamisi mwezi (30 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (20 Agosti 2020m).

Akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi inayo julikana na mingine haijulikani kwa wananchi kiukamilifu, lakini yote inaingia ndani ya kapu la (viwanda vya Iraq) bila shaka inahudumia soko la ndani”.

Akabainisha kuwa: Miradi hiyo ni muhimu sana, kuna haja ya kupewa ushirikiano na raia wa Iraq pamoja na viongozi wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: