Rais wa mtandao wa habari Al-Iraqiyyu ametembelea miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Rais wa mtandao wa habari Al-Iraqiyyu Dokta Nabiil Jaasim ametembelea miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Alkhamisi mwezi (30 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (20 Agosti 2020m), akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Ataba takatifu.

Tumeongea na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kuwa: “Ziara hii imelenga kukagua miradi, tumetembelea hospitali ya rufaa Alkafeel, Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji, majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi, kituo cha maegesho ya magari Alkafeel na shirika la Khairul-Juud”.

Akaongeza kuwa: “Ziara ilikuwa nzuri, nayo ni mwanzo wa ziara zingine zinazo lenga kuonyesha mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuyaingiza kwenye kapu la (viwanda vya Iraq)”.

Baada ya kumaliza kutembelea miradi, rais wa mtandao wa habari Al-Iraqiyyu amembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na katibu mkuu pamoja na viongozi wengine, akasifu kazi kubwa inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya kwenye sekta mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: