Kulinda afya za mazuwaru: Kubadilisha bendera za kubba mbili kutoa nyekundu na kuweka nyeusi kwa shughuli fupi kama ishara ya kuanza mwezi wa Muharam 1442h

Maoni katika picha
Kila mwaka hukumbukwa masomo ya harakati ya Imamu Hussein na ushujaa wake mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Muharam, imekuwa desturi ya wairaq kushusha bendera nyekundu iliyopo juu ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kupandisha bendera nyeusi kama ishara ya kuanza maombolezo hayo, shughuli hiyo hufanywa katika mazingira ya huzuni na majonzi makubwa.

Utamaduni wa kubadilisha bendera ulianza miaka mingi iliyopita, na umekua ukiendelezwa na kila uongozi wa Ataba, watu wamezowea kuona bendera ikibadilishwa dakika chache baada ya kuingia mwezi wa Muharam na baada ya adhana ya Magharibi, hususan wakati wa utawala wa dikteta aliye zuwia harakati zote za uombolezaji.

Idara za Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya baada ya dikteta kuangushwa na waumini kupata uhuru zimeamua kuendeleza ada hiyo, kama ishara ya kuujulisha ulimwengu kuingia mwezi huu wenye tukio kubwa lililobadilisha historia, na kuulinda uislamu kwa maelfu ya miaka hadi siku ya kiyama, shughuli ya kubadilisha bendera hupambwa na kaswida za kuomboleza pamoja na mawaidha, na huhudhiriwa na maelfu ya mazuwaru, aidha hupambwa na waimbaji wa kikabila pamoja na gwaride la jeshi la Iraq na mambo mengine yanayo ashiria ukubwa wa jambo hilo.

Shughuli ya kubadilisha bendera ilianza mwezi wa Muharam wa mwaka 1426h sawa na mwezi wa pili mwaka 2005m, na kuhudhuriwa na watu wachache, ikaendelea kufanywa kila mwaka huku idadi ya watu wanao shiriki ikiongezeka kila mwaka hadi mwaka jana 1441h, ikawa tayali inahudhuriwa na watu wengi, idadi ya wahudhuriaji imesha fika maelfu katika mwaka 2019m.

Kwa kuwa shughuli hii kwa sasa inahudhuriwa na mamilioni ya watu, na mazingira yetu ya sasa hayaruhusu mikusanyiko ya watu kwa sababu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kulida usalama wa afya zao, chini ya maelekezo ya wizara ya afya na shirika la afya duniani, sambamba na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufanya maadhimisho ya Husseiniyya pamoja na kufuata maelekezo ya wizara ya afya, mwaka huu Muharam 1442h sawa na (20/08/2020m) shughuli haikua sawa na miaka mingine, zimebadilishwa bendera za kubba mbili na kuimbwa kaswida ya (ewe mwezi wa Ashura) ya marehemu Hamza Swaghiir pamoja na kuzima taa nyeupe na kijani katika eneo la katikati ya haram mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya na kuwasha taa nyekundu.

Bendera nyekundu inamaanisha kuwa mwenye kaburi hili aliuwawa na bado hajalipiziwa kisasi kwa mujibu wa desturi za waarabu, na bendera nyeusi inaashiria huzuni na majonzi, kila mwaka unapoingia mwezi wa Muharam hushushwa bendera nyekundu na kupandishwa nyeusi ambayo hukaa hadi mwezi mosi Rabiul-Awwal, ndipo hurudishwa bendera nyekundu.

Wanahistoria wanasema kuwa mtu wa kwanza aliyepandisha bendera nyekundu alikuwa ni mzee wa kabila la bani Asadi, baada ya Mukhtaaru Thaqafi kujenga malalo ya Imamu Hussein (a.s) ndipo ikapandishwa bendera nyekundu kwenye kubba lake, tangu kipindi hicho imekuwa ikiwekwa bendera mpya kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: