Katika utekelezaji wa masharti ya afya ya mikusanyiko, mawakibu za waombolezaji zimeanza kuomboleza

Maoni katika picha
Asubuhi ya siku ya kwanza ya Muharam 1442h sawa na tarehe (21 Agosti 2020m) maukibu za waombolezaji za Karbala zimeanza kuomboleza, chini ya utekelezaji wa maelekezo ya idara ya afya, kwa washiriki wa maukibu na watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, maelekezo yote yaliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu pamoja na wizara ya afya yanatekelezwa, ikiwa ni pamoja na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu, na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, bila kusahau uvaaji wa barakoa ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimeshuhudia kuwasili kwa mawakibu hizo moja baada ya nyingine kwa kufuata ratiba kama ilivyo pangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya.

Matembezi ya mawakibu hizo yanaanzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuishia kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Sayyid Hashim Mussawi makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya amesema kuwa: “Kitengo chetu kilifanya makubaliano na viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya ya kuomboleza na tukaandaa ratiba ya uingiaji wa mawakibu ndani ya siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam, kila maukibu itaingia na idadi maalum ya watu watakao fuata kanuni zote za kujikinda na maambukizi, watafanya majlisi ndani ya haram kwa muda wa robo saa, ili kutoa nafasi kwa maukibu nyingine na kuepusha msongamano”.

Tambua kuwa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya usafi mkubwa na kuchukua tahadhari zote za afya, ili kuhakikisha usalama wa mawakibu hizo sambamba na kuainisha milango maalum itakayo tumika katika kuingia na kutoka, ikiwa ni pamoja na kuzisimamia kuanzia mwanzo hadi mwisho, na kuweka kikosi cha watumishi kinacho puliza dawa kwenye makundi ya waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: