Kituo cha utamaduni wa familia kinaendesha ratiba ya Ashura iitwayo (Miezi katika mhimili wa utukufu) kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha ratiba kwa njia ya mtandao iitwayo (Miezi katika mhimili wa utukufu), kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Muharam na kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake katika vita ya Twafu, huu ukiwa ni muendelezo wa kuangazia baadhi ya yaliyotokea.

Mkuu wa kituo Ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunaendesha ratiba hii kwa ajili ya kuhuisha tabia njema kwenye nafsi zetu na kusoma mafundisho yanayo patikana katika harakati ya Imamu Hussein (a.s) na malengo yake matukufu yanayo mrudisha mwanaadamu katika asili, na kuifanya jamii kuwa na maadili ya ubinaadamu bila kujali tofauti zao”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba hii itadumu siku zote za Muharam sambamba na kuangazia mashujaa wa vita ya Twafu ili tuweze kusoma kwao na kufuata mwenendo wao, tutatoa link yenye kurasa za kitabu cha mmoja wa mashahidi wa vita ya Twafu, pamoja na maswali yatakayo mchochea msomaji kutafakari, ili kushiriki fungua link maalum kuhusu balozi wa Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil (a.s).

Kujisajili fungua link ifuatayo: https://forms.gle/WmvdcpUPUjkYEeyy5

Kwa maelezo zaidi angalia:

Instagram

Telegram

Facebook
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: