Vituo vya Ashura: kitu gani kilitokea mwezi tatu Muharam?

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa katika siku kama ya leo mwezi tatu Muharam mwaka 61h, Ubaidu Llahi bun Ziyadi gavana wa Kufa alituma wapiganaji (wanajeshi) elfu thelathini, na inasemekana walikua elfu arubaini, chini ya uongozi wa Omari bun Saadi kwend Karbala, kupigana na Imamu Hussein (a.s), akamuahidi kumpa ugavana wa jimbo la Rai iwapo akifanikiwa kumuuwa Imamu Hussein (a.s), jeshi likawasili Karbala katika siku kama ya leo.

Omari bun Saadi akutana na Imamu Hussein (a.s):

Omari bun Saadi alikutana na Imamu Hussein (a.s) akamuuliza sababu za kuja kwake Kufa, Imamu Hussein (a.s) akamjibu: (Watu wamji huo wameniandikia barua za kuniita, kama hamtaki naweza kurudi).

Barua ya Omari bun Saadi kwa ibun Ziyaad:

Omari bun Saadi alimuandikia barua bun Ziyaad ya kumuambia mazungumzo yake aliyofanya na Imamu Hussein (a.s), ya kwamba ampe nafasi Imamu Hussein (a.s) ya kurudi na wala asipigane nae.

Barua ya ibun Ziyaad kwa Omari bun Saadi:

Ibun Ziyaad alituma barua ya majibu kwa Omari bun Saadi iliyopelekwa na Shimri bun Dhijaushen (laana iwe juu yake), na akamuambia Shimri; amuambie Hussein na watu wake wautii utawala wangu, wakikubali awalete kwangu kwa amani, na wakikataa awauwe, Omari akitekeleza agizo hili msikilize na umtii na kama akikataa muuwe unitumie kichwa chahe na uongoze jeshi, barua ilikuwa imeandikwa hivi: (Mimi sikukutuma kwa Hussein ukawe ngao yake, wala kuongea nae, wala kumpa amani na kumbakisha hai, au kumuombea msamaha kwangu na kuwa msemaji wake, iwapo Hussein na watu wake watautii utawala wangu walete kwangu kwa amani na wakikataa watese, uwauwe na udhalilishe maiti zao, hakika wao wanastahiki kufanyiwa hivyo, baada ya kuuwawa Hussein amrisha farasi zikanyage kanyage kifua chane na mbongo wake, ukitii amri yangu nitakupa zawadi ya kamanda mtiifu, na ukikataa achana na kazi yangu pamoja na jeshi langu, uongozi wa jeshi utachukuliwa na Shimri bun Dhijausheni, hakika yeye tumempa maagizo yetu, wasalaam).

Msimamo wa Omari bun Saadi:

Omari bun Saadi alipokea barua na akaisoma, akaanza kupambana na nafsi yake kati ya kumkabili Imamu Hussein (a.s) na kumuuwa, ili apewe ugavana na heshima kubwa mbele ya viongozi wake, na baina ya kukubali kufanya dhambi hiyo kubwa, nafsi yake ikampambia kuchagua uongozi na mali, akakubali kuongoza vita ya kumuuwa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake huku akisaidiwa na Shimri bun Dhijaushen.

Ibu Saadi akamlazimisha Imamu Hussein (a.s) ajisalimishe na akamzuwia kutumia maji, Imamu (a.s) alikataa kumtii pamoja na ukubwa wa jeshi la maadui na uchache wa watu wake, akasema maneno yafuatayo: (Tambueni hakika muovu mtoto wa muovu ametupa moja ya mambo mawili, baina ya kupigana vita au udhalili, uwe mbali nasi udhalili, Mwenyezi Mungu hataki tuwe madhalili pamoja na Mtume wake na waumini, nyuoyo safi na takatifu…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: