Ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niyaba inasomwa kila siku na itahitimishwa kwa ziara maalum siku ya mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Hashim Shami, amesema kuwa kundi la masayyid linafanya ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niyaba ya watu waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel pamoja na swala ya rakaa mbili.

Akaongeza kusema kuwa: “Ziara itakayo somwa ni ziara ya Ashura ambayo husomwa kwa ajili ya Imamu Hussein kwa mbali au karibu, kupitia ziara hiyo wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hujikumbusha yaliyo mpata Imamu wao na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake katika ardhi ya Karbala siku ya Ashura, nayo hunasibishwa na Imamu Baaqir (a.s), inahadhi maalum na usomwaji wake huhimizwa mara nyingi, hususan katika mwezi wa msiba mwezi wa Muharam, pamoja na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusomwa ziara hizo huswaliwa rakaa mbili na kumuomba Mwenyezi Mungu akidhi haja na kurahisisha mambo pamoja na kuondoa balaa”.

Akabainisha kuwa: “Kazi hii imeanza tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na itaendelea hadi siku ya tisa, itahitimishwa kwa kusoma ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenye malalo zao takatifu siku ya kumi”.

Akamalizia kwa kusema: “Mazuwaru wanaopenda kufanyiwa idada hizi kwa niaba, na kupata thawabu na malipo ya ibada hizo kwa idhini wa Mwenyezi Mungu, wanaweza kujisajili kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/ ".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: