Vituo vya Ashura: Mwezi nne Muharam Ubbaidullahi bun Ziyaad afunga mipaka ya mji wa Kufa na awazuwia wakazi wa mji huo kwenda kumnusuru Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi nne Muharam mwaka (61h) Ubaidullahi bun Ziyaad Gavana wa kufa alitoa hutuba kali na kuonya yeyote atakaemsaidia Imamu Hussein (a.s) atauwawa, na Qadhi Sharihi akasoma fatwa ya kuhalalisha kuuwawa Imamu Hussein (a.s), na kufunga njia zote zinazo ingia Kufa, ili kuwazuwia watu wa Kufa na maeneo mengine wasiende kumnusuru Imamu.

Vitisho na mateso makali ndio njia aliyotumia ibun Ziyaad kwa wafuasi wa Imamu Hussein na akawapa matumaini na mali watu walio muunga mkono, watu wenye Imani dhaifu akawavuta kwa mali, huku viongozi wa makabila akiwapa vyeo na mali nyingi, na wale waliokuwa na imani waliteswa na kufungwa jela, wengi walipo toka jela walianzisha harakati ya watubiao (Tawabiina), kama vile Suleimani bun Swardi Alkhuzaai na wafuasi wake.

Viongozi wa koo waliokuwa wafuasi wa Imamu (a.s) waliteswa na kufungwa jela, tunajua kuwa aliyekuwa akishawishi watu katika njia sahihi ni mtu mwenye hadhi kubwa, viongozi wa koo walikuwa wamegawika baina ya umawiyyina na Alawiyyina, Ibun Ziyadi aliwatumia kumdhibiti kila aliye mhalifu.

Kila kabila lilipoteza kiongozi wake hivyo wakadhofika na kukosa msimamo, haya ndio yaliyofanywa na ibun Ziyaad kwa uchache, alimkamata kila anayemhalifu na aliweka majasusi kila sehemu, aliweka watu kwenye njia zote zinazo ingia kufa walio wahofisha watu kwa kuwaambia kuwa kunajeshi kubwa linakuja kumsaidia kutoka Sham, katika mazingira hayo mtu dhaifu aliyebaki mpweke hawezi kuwa na msimamo lazima atatetereka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: