Vituo vya Ashura: Mwezi tano Muharam kukamilika idadi ya jeshi lililokwenda kumpiga Imamu Hussein (a.s) na kuimarisha vizuwizi kwa watu wa Kufa wasiende kumnusuru

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa siku ya mwezi tano Muharam mwaka 61 hijiriyya, jeshi la maadui lilikamilika na kukusanyika katika ardhi ya Karbala, wakiwa wamejiandaa kumshambulia Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake.

Wapelelezi wa Ubaidullahi bun Ziyadi waliuzunguka mji wa Kufa na wakazuwia wakazi wa mji huo wasiende kumnusuru Imamu Hussein (a.s) kwa kuweka vikosi vya askari pembezoni mwa mji huo.

Akaendelea kutuma watu kwa wakazi wa Kufa na kuwaamrisha wamtii pamoja na kutoa onyo kali kwa yeyote atakae asi, pamoja na kuwataka wajiunge na jeshi la Yazidi (laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake), aidha ibun Ziyadi aliendelea kutuma wanajeshi kwa ibun Saadi hadi idadi yao ikafika elfu thelathini, baadhi ya riwaya zinasema kuwa jeshi lililokwenda kupigana na Imamu Hussein (a.s) lilikuwa na wapiganaji elfu thelathini wapanda farasi na watembea kwa miguu, ibun ziyadi aliweka walinzi sehemu zote za milima ya Kufa, kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakaekwenda kumsaidia Imamu Hussein (a.s).

Upande wa watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake imazi zao zilikuwa zinaongezeka na kuwa na msimamo imara wa kumnusuru mtoto wa binti wa Mtume (s.a.w.w) hadi teno la mwisho la damu, wala hawakutishika au kuogopa ukubwa wa jeshi linalowazunguka, bali liliwaongeza ujasiri wa kuendelea kumlinda Imamu Hussein (a.s), kama alivyo sema Imamu mwenyewe (a.s) kuwa: (Hakika mimi sitambui wafuasi bora na waaminisu kushinda wafuasi wangu, wala watu wa nyumba wema na wenye mshikamano kuliko watu wa nyumba yangu, Mwenyezi Mungu akulipeni kheri).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: