Kituo cha utamaduni wa familia kimezindua jukwaa la kielektronik la mafunzo ya wanawake

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimezindua jukwaa la kielektronik la kutoa mafunzo maalum kwa wanawake, katika kuhakikisha unapatikana utulivu wa nafsi kwenye familia na kutibu matatizo ya kijamii na kimalezi pamoja na kinafsi ndani ya jamii, sambamba na kuendeleza mawasiliano kwenye kipindi hiki muhimu, kwa kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya kifamilia yanayo endana na kila umri wa mwanamke chini ya usimamizi wa jopo la wataalam.

Mkuu wa kituo hicho Ustadhat Asmahani Ibrahim akasema kuwa: “Jukwaa hilo linapatikana kupitia link ifuatayo: https://t.me/thaqafaasaria_platform7, tutatoa mafunzo maalum kuhusu, nafsi, familia, ndoa, ujana, utoto na uzee, tutajibu mahitaji ya msingi ya mwanaadamu na kumuwezesha kukamilisha dhati yake na maendeleo”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya malengo ya kuanzishwa kwa kituo hiki ni kuwasiliana na familia pamoja na viongozi wa nyumba sambamba na makundi yote ya jamii, aidha kukutana nao moja kwa moja na kujibu maswali yao na kutatua changamoto za kifamilia, hakika jamii zinachangamoto nyingi, lakini katika mazingira haya na ukizingatia maelekezo ya afya ya kuzuwia mikusanyiko ya watu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi, tumelazimika kutumia majukwaa ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii ili kuwasilisha mambo yanayo hitajiwa na kundi hili”.

Kituo kimetoa wito kwa kila anaependa kushiriki katika mradi huu kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii ya kituo (Viber, Whatsap, Telegram), au kujiunga kupitia link ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: