Atabatu Abbasiyya imeimarisha mfumo wa kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha mfumo wa kujikinga na maambukizi wakati wa matembezi ya mawakibu zinazo shiriki katika uombolezaji, kitengo cha usimamizi wa haram takatifu kimeweka utaratibu maalum wa kutembea, na kimeweka alama zinazo onyesha umbali unaotakiwa baina ya mtu na mtu ili kulinda usalama wao.

Haya yamesemwa na makamo rais wa kitengo hicho Uastadh Zainul-Aabidina Quraishi, akaongeza kuwa: “Mawakibu za kuomboleza zinapo karibia kuingia kwenye haram tukufu, watumishi wa kitengo chetu chini ya maelekezo ya Ataba tukufu wameweka mfumo wa kuwalinda waombolezaji na maambukizi kwa kiwango kikubwa, wameweka alama zinazo saidia kupatikana umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu, leo tumeweka alama za mistari (10) itakayo tumiwa na watembeaji, umbali wa mstari mmoja na mwingine ni mita moja, kuanzia maukibu inapoanza kuingia ndani ya haram hadi itakapo toka, kila mstari una alama zenye ukubwa wa (sm30) zinazo onyesha sehemu ambayo mtu anatakiwa kusimama, kutoka alama moja hadi nyingine kuna umbali wa mita moja pia, huo ndio umbali uliopasishwa na idara ya afya, alama hizo zimewekwa kwa kutumia gundi madhubuti na yenye muonekano mzuri”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ndani na nje ya haram tukufu, mambo yote yanafanywa chini ya usimamizi wa idara ya madaktari na maelekezo ya wizara ya afya, na jambo hili ni moja ya shughuli nyingi za kulinda usalama wa afya za mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: