Sayyid Murtadhwa Ghalibi amesema kuwa: “Kikosi chetu kimezowea katika kila msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, husambazwa Skaut wa kitengo cha Aljawaalah kwa ajili ya kufanya shughuli za uokozi wa mazuwaru na kutoa msaada wa haraka utakao hitajika na zaairu, lakini mwaka huu kutokana na kuwepo janga la Korona kazi yake imetofautiana na miaka mingine, mwaka huu tunafanya mambo yafuatayo:
- - Kushindikiza mawakibu za waombolezaji zinazo ingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kupulizia dawa vikundi vya watu wanaoshiriki kwenye maukibu hizo, kwa kutumia dawa zilizo pasishwa na idara ya madaktari wa Ataba tukufu, kazi hiyo inaanzia wakati maukibu zinapo karibia kuingia ndani ya haram na inaendelea hadi zitakapo toka na kushindikizwa hadi kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.
- - Kuna kikosi cha wanaskaut wa kitengo cha Aljawaalah waliopewa jukumu la kutoa elimu na kugawa vipeperushi vinavyo eleza hatari ya maambukizi ya virusi vya Korona na namna ya kujikinga navyo”.
Kumbuka kuwa kikosi cha mafunzo na uokozi kimesha okoa maisha ya mamia ya mazuwaru kwenye ziara zilizo pita na kuhakikisha usalama wao pamoja na kuweka mazingira rafiki, sambamba na kuzuwia misongamano ya mazuwaru, na kupeleka watu wenye matatizo ya afya kwenye hospitali za karibu kwa kutumia magari maalum ya wagonjwa.