Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu wameanza kutekeleza mkakati wao wa ziara ya mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wameanza kutekeleza mkakati wao malum wa ziara ya usiku wa mwezi kumi Muharam na mchana wake, mkakati wa kuratibu matembezi na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi kwa ajili ya usalama wa waombolezaji.

Tumeongea na makamo rais wa kitengo hicho Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema: “Watumishi wa kitengo chetu wametandika busati lekundu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika eneo linalo kadiliwa kuwa na ukubwa wa mita (5250), juu ya busati hilo kuna alama zinazo onyesha sehemu ambayo mtu anatakiwa kusimama kwa kuzingatia umbali unaotakiwa na idara za afya, kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa milango maalum itakayo tumiwa na waombolezaji wa matembezi ya Towareji katika kuingia na kutoka”.

Kuhusu shughuli za kujikinga na maambukizi amesema kuwa: “Kuna kikosi kazi maalum cha vijana wa Skaut (Aljawaalah) kinacho puliza dawa muda wote ndani ya haram tukufu, kuna vifaa zaidi ya (20) tumeviweka milangoni ambavyo vinapuliza dawa kila kitu kikiwa umbali wa mita sita”.

Akaendelea kusema: “Aidha tunashirikiana na ndugu zetu watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu kasimamia matembezi ya mawakibu kuanzia zinapo ingia hadi zinapo toka”.

Tambua kuwa kitengo cha kusimamia haram tukufu kinamajukumu mengi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kufagia, kupiga deki, kutandika miswala na zinginezo, kazi zao huongezeka zaidi wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: