Katika kuhitimisha uombolezaji wa matembezi ya Towareji: Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa hatua ya kwanza ya mkakati wake na imeanza hatua ya pili

Maoni katika picha
Katika kuhitimisha uombolezaji mkubwa duniani wa matembezi ya Towareji ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu, Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi na usalama pamoja na huduma za afya, katika ziara ya mwezi kumi Muharam (1442h).

Shughuli zote zilizo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kuanza kutekelezwa tangu siku kumi zilizo pita zimefanyika kwa mafanikio, ikiwa ni pamoja na kuhitimisha matembezi makubwa zaidi duniani (matembezi ya Towareji), yamefanyika bila kutokea tatizo lolote, makundi ya mazuwaru na waumini wa Karbala wameshiriki kwenye matembezi hayo, na kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa kuuwawa babu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake watakatifu na wafuasi wake, muda uliotumika kufanya matembezi hayo ulikuwa zaidi ya saa tatu, matembezi yamefanyika kwa utaratibu mzuri.

Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wahudumu wa afya, sambamba na watu waliojitolea kufanya kazi pamoja na wahudumu wa Ataba tukufu, huu ni muendelezo wa mafanikio yaliyo tangulia ya uratibu mzuri wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kukamilika kwa matembezi hayo kumepelekea kuanza hatua ya pili ya kufanya usafi ndani na nje ya haram pamoja na kuondoa mchanga milangoni na sehemu zote zilizo tumiwa na waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: