Vituo vya Ashura: Mwezi kumi na tatu Muharam kuzikwa mwili wa Imamu Hussein (a.s) na mashahidi wengine wa Twafu

Maoni katika picha
Watu wa historia wanasema kuwa mwezi kumi na tatu Muharam mwaka 61h, baada ya muili wa Imamu Hussein (a.s) kubaki juu ya udongo wa Karbala bila kichwa pamoja na familia yake na wafuasi wake walio uwawa pamoja nae wakipigwa na jua, huku familia zao na watoto wao wakiwa mateka pamoja na bibi Zainabu na Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s), wanawake wa bani Asadi walikuta miili ya watu ikiwa imetapakaa bila kuoshwa wala kuzikwa, wakaenda haraka kuwaambia wanaume walichokiona katika ardhi ya Karbala, nao wakaenda kuangalia miili hiyo mitakatifu.

Wakaukuta muili wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na miili mingine haina vichwa, katika mazingira yanayoweza kumzeesha mtoto mdogo, wakataka kuanza kuuandaa muili wa Imamu Hussein (a.s) na kuuzika, mara akatokea Imamu Zainul-Aabidina (a.s), alifika kwa muujiza wa kukunja ardhi.

Shekh Mufidi anasema: Alipofika Sajjaad (a.s) aliwakuta bani Asadi wamekusanyika mbele ya maiti, wametahayari hawajui cha kufanya, hawatambui maiti hii ya nani na ile ya nani, kwani zilikua hazina vichwa, pia walikua wanajiuliza familia za watu hao ziko wapi na wakina nani! Alipo fika (a.s) akawaambia kuhusu miili hiyo mitakatifu pamoja na kuwatajia majina yao na koo zao, akawatambulisha bani Hashim na wafuasi wa Imamu (a.s), wakalia sana.

Kisha Imamu (a.s) akaenda kwenye muili wa baba yake, akaukumbatia na kulia sana, halafu akaenda sehemu ya kaburi akaondoa mchanga kidogo, akakuta kaburi limesha chimbwa, akamshika mgongoni na akasema: (Bismillahi wa fii sabili Llahi wa ala milati Rasulullahi, swadaqa Llahu wa Rasuluhu, maashaa-allahu laa haula wa laa quwata illaa billahil-aliyyul-adhiim), akamteremsha kaburini peke yake bila kusaidiwa na bani Asadi, akawaambia: (Ninao wanaonisaidia), alipo muweka kwenye mwanandani akaweka shavu kwenye shingo lake takatifu kisha akasema: (Imefaulu ardhi inayobeba muili wako mtakatifu, hakika dunia baada yako ni giza, na akhera inangáa nuru yako, usiku unagiza, na huzuni ya kudumu, au Mwenyezi Mungu awape watu wa nyumbani kwako nyumba ambayo wewe unaenda kuishi, amani iwe juu yako kutoka kwangu ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na rehema zake na baraka zake), halafu akaandika juu ya kaburi: Hili kaburi la Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), aliyeuwawa akiwa ugenini akiwa na kiu.

Kisha akaenda kwa Ammi yake Abbasi (a.s), akamkuta katika hali ambayo iliwaumiza malaika wa mbinguni, na ikaliza mahuruaini katika vyumba vya peponi, akasema: (Dunia baada yako siko kitu ewe mwezi wa bani Hashim, nakutakia amani ewe shahidi na rehma na baraka za Mwenyezi Mungu).

Akachimba kaburi na akamzika peke yake kama alivyo fanya kwa baba yake, akawaambia bani Asadi: (Ninao wanaonisaidia), ndio.. aliwaachia bani Asadi wakaendelea kuzika mashahidi wengine, akawaonyesha sehemu mbili za kuchimba kaburi, sehemu ya kwanza wakazikwa bani Hashim na sehemu ya pili wakazikwa wafuasi wa Imamu (a.s), muili wa Hurru Riyahi ukaenda kuzikwa sehemu nyingine na familia yake, kaburi lake lipo huko hadi sasa, baada ya Imamu (a.s) kumaliza kuzika alirudi Kufa kuungana na mateka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: