Inatokea hivi sasa: Msafara wa waombolezaji wa kabila la bani Asadi bamoja na makibila mengine unaomboleza kuzikwa miili mitakatifu ya mashahidi wa Twafu

Maoni katika picha
Mji mtukufu wa Karbala unashuhudia msafara (maukibu) kubwa ya bani Asadi pamoja na makabila mengine ya Iraq, katika kumbukumbu ya kuzikwa muili mtakatifu wa bwana wa mashahidi na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake watukufu walio uwawa pamoja nae katika jangwa la Karbala.

Imekuwa ni utamaduni wa maombolezo haya kutanguliwa na wanawake wa bani Asadi hadi kwenye kaburi la bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kukumbuka yaliyojiri mwezi kumi na tatu Muharam mwaka wa 61h.

Mwezi kumi na tatu Muharam ni miongoni mwa siku muhimu katika nyoyo za watu wa Karbala, na moja ya sehemu kubwa ya maombolezo ya Ashura, kwani ni siku ya kukumbuka kuzikwa kwa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, baada ya kukaa siku tatu juu ya jangwa la Karbala wakipigwa vumbi.

Riwaya zinasema kuwa siku ya tatu baada ya kuuwawa Hussein (a.s) na familia yake, kundi la wanawake wa bani Asadi lilifika eneo hilo, wakakuta miili imekatwakatwa na haina vichwa, imeachwa bila kuzikwa, wakaenda kuwaambia wanaume, ambao walifika haraka eneo hilo wakiwa na vifaa vya kuzikia, wakasimama wakiwa wametahayari kutokana na walicho kiona, maiti zikiwa zimejaa vumbi na hazina vichwa, wakati wakiwa wanaulizana cha kufanya mara aliwasiri Imamu Zainul-Aabidina (a.s), akajitambulisha kwao na akawaomba wamsaidie kuzika maiti zile, wakashirikiana na Imamu kuzika na likawa hilo ni tukio lao la kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: