Kwa picha: Bani Asadi wakiwa na makabila mengine ya wairaq wanahuisha kumbukumbu ya maziko ya miili mitakatifu ya mashahidi wa Twafu

Maoni katika picha
Maukibu ya waombolezaji wa kabila la bani Asadi pamoja na makabila mengine ya wairaq baada ya Adhuhuri ya Jumatano mwezi (13 Muharam 1442h) sawa na tarehe (2 Septemba 2020m) zimehuisha kumbukumbu ya kuzikwa miili ya mashahidi wa Twafu (a.s).

Matembezi ya maukibu hiyo yameanzia pale walipozowea kuanzia kila mwaka, katika eneo la (bwana wa ukaribu) karibu na makaburi ya zamani, wametembea wakiwa wanaimba kaswida za huzuni na majonzi.

Kisha wakaingia katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), halafu wakaingia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na wakaishia katika malalo ya mbeba mbendera Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maukibu za waombolezaji ziliendelea kumiminika kwa muda mrefu, huku maukibu za kutoa huduma zikiendelea kuwahudumia, aidha kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya kila kiwezalo katika kuhakikisha matembezi hayo yanafanyika kwa amani na utulivu.

Watu wa Karbala wamezowea kufanya matembezi haya wakitanguliwa na watu wa kabila la bani Asadi, lililopata utukufu mwaka (61h) wa kushirikiana na Imamu Sajjaad (a.s) kuzika miili ya mashahidi wa Twafu.

Katika maombolezo hayo hushiriki makabila mengine kutoka nje ya mkoa wa Karbala, huja makundi kwa makundi wakiwa wamevaa nguo za asili ya kiarabu, wakiwa wametanguliwa na makundi ya wanawake kutoka ndani na nje ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: