Vituo vya Asura: Zainabu Kubra na muovu ibun Ziyadi.. akukose mama yako ewe ibun Marjana, sikuona ispokua wema.

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa katika siku kama hizi mwaka (61h), waliwasili mateka wa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mji wa Kufa baada ya tukio la Ashura, Ubaidullahi bun Ziyadi Gavana wa Yazidi aliamrisha aletewe kichwa cha Imamu Hussein (a.s), akaanza kukichoma choma katika midomo yake mitakatifu na fimbo, kisha wakaletwa mateka mbele yake wakitanguliwa na bibi Zainabu (a.s).

Shekh Mufidi katika kitabu cha (Irshadi) anasema: (Familia ya Hussein (a.s) iliingizwa kwa ibun Ziyadi, akiwemo bibi Zainabu dada wa Imamu Hussein (a.s) akakaa pembeni ya Qasri, na kujifunika kipande cha nguo yake.

Ibun Ziyadi akasema: Nani huyu aliyekaa pembeni akiwa kazungukwa na wanawake?! Zainabu hakumjibu. Akauliza mara ya pili na mara ya tatu.

Wakamjibu baadhi ya watu aliokuwa nao: Huyu ni Zainabu mtoto wa Fatuma mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ibun ziyadi akamuelekea, na akamuambia: Kila sifa nyema anastahiki Mwenyezi Mungu aliye kufedhehesheni na kukuuweni na kuonyesha uongo wenu. Bibi Zainabu akasema: Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu aliyetukirimu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kututakasa na uchafu, hakika muovu hufedheheka na kukadhibishwa, wala sio sisi. Ibun Ziyadi akasema: Umeona jinsi Mwenyezi Mungu alivyo wafanya watu wa nyumbani kwako?

Akasema: Sijaona ispokua wema, hawa ni watu walioandikiwa kifo, wamepigana na kufa shahidi, Mwenyezi Mungu atawakutanisha wewe na wao na mtahojiana mbele yake, tutaona nani atakaefaulu siku hiyo, amekukosa mama yako ewe ibun Marjana!! Ibun Marjani akakasirika, Amru bun Haarith akamuambia: Ewe kiongozi, hakika huyu ni mwanamke, na mwanamke hachukuliwi hasira kwa maneno yake. Ibun Ziyadi akasema: Mwenyezi Mungu kauponya moyo wangu kutokana na muovu wako Hussein na waasi katika familia yako. Bibi Zainabu akalia, na akasema: Hakika umeuwa pambo la macho yangu na umevunja ngome yangu na kungóa msingi wangu, kama hiyo ndio ponyo yako basi umepona.

Ibun Ziyadi akasema: Hii ni Sajaa (ajabu), hakika baba yake Sajaa alikuwa mshairi.

Kisha ibun Ziyadi akamgeukia Ali bun Hussein akamuuliza: Nani wewe?

Akasema (a.s): Mimi ni Ali bun Hussein. Akasema: Mwenyezi Mungu hajamuuwa Ali bun Hussein? Akasema (a.s): Nilikuwa na ndugu anaitwa Ali bun Hussein ameuliwa na watu. Ibun Ziyadi akasema: Bali ameuliwa na Mungu.

Imamu (a.s) akasema: (Mwenyezi Mungu huchukua nafsi wakati wa kifo chake). Ibun Ziyadi akachukia kwa majibu ya Ali (a.s), akamwita muuwaji akamuambia mkate shingo lake. Bibi Zainabu (a.s) akamkubatia mtoto wa kaka yake, na akasema: (Ewe ibun Ziyadi inatosha kumwaga damu zetu, wallahi sitamuachia ukimuuwa uniuwe pamoja nae).

Ibun Ziyadi akaangalia kisha akasema: Ajabu sana undugu! Mimi sikudhani kama angetaka kuuwawa pamoja nae, muacheni.

Kisha akaamuru Ali bun Hussein na familia yake wapelekwe kwenye nyumba iliyokuwa pembeni ya msikiti mkubwa, Zainabu binti Ali akasema: (Asiingie kwetu ispokua mama wa mtoto mateka, hakika wao wametekwa kama sisi).

Katika majadiliano hayo mafupi ikawa imejulikana kheri na shari, na mwema na muovu, utukufu na uchafu na baina ya watoto waliokulia katika nyumba ya wahyi na muovu mtoto wa muovu! Pande zote mbili zikajulikana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: