Baada ya kumaliza shughuli za uombolezaji katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam: Uwanja wa katikati ya haram mbili unashuhudia opresheni kubwa ya usafi

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanafanya opresheni kubwa ya usafi katika eneo hilo hadi kwenye maeneo yaliyo pauliwa na pembezoni mwake, baada ya kumaliza shughuli za uombolezaji wa siku ya mwezi kumi na tatu Muharam (maombolezo ya bani Asadi).

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wetu walifanya usafi na kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona siku chache kabla ya kuingia mwezi wa Muharam, na wakaendelea kufanya hivyo hadi siku ya mwezi kumi Muharam, hivi sasa wameondoa busati lekundu lililotandikwa kwa ajili ya kuonyesha ubali ambao mtu anatakiwa kusimama kati yake na mtu mwingine, kazi hiyo imehitimishwa na kazi nyingine iliyo anza baada ya kuisha maombolezo ya bani Asadi, ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya maombolezo ya Towareji, kitengo kimefanikiwa kurudisha mazingira ya kawaida katika eneo hilo ndani ya muda mfupi”.

Mussawi akasema: “Kazi hii imefanywa na watumishi wa idara ya usafi, imehusisha uwanja wa katikati ya haram mbili, eneo lililo pauliwa, sehemu za maji, kuta na bustani, wametumia vifaa vya usafi na vile vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kama ilivyo elekezwa na idara ya afya”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kumaliza ziara yeyote kubwa, watumishi wake hufanya usafi wa kina, kwa ajili ya kuweka muonekano mzuri na kurudisha mazingira kama yalivyokuwa, huo ndio mkakati wake wa kiutendaji baada ya kila ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: