Waziri wa mafuta ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kasifu ubora wa huduma wanazo pewa mazuwaru

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa mwezi (15 Muharam 1442h) sawa na tarehe (4 Septemba 2020m) waziri wa mafuta wa Iraq Sayyid Ihsani Abduljabbaar, ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia ubora wa huduma wanazo pewa mazuwaru wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi.

Baada ya kumaliza kufanya ibada ya ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), waziri amekutana na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi, na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya utendaji.

Katika mahojiano maalum tuliyo fanya na waziri amesema kuwa: “Lengo ka ziara hii ni kuangalia huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Wizara ya mafuta inamchango mkubwa katika ziara ya Ashura kwa kuhakikisha mafuta ya aina mbalimbali yanapatikana bila usumbufu katika kipindi hicho, leo tumekuja kuangalia na kujiridhisha ubora wa huduma tuliyo toa, na kusikiliza maoni kama yapo, pamoja na kujifunza baadhi ya mambo kwa ujumla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: