Chuo kikuu cha Alkafeel kinaomboleza tukio la Twafu na mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s) ya kudumu

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya majlisi ya kuomboleza tukio la Twafu na kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (r.a), kwa kufuata maelekezo yote ya afya yaliyo himizwa na Marjaa Dini mkuu na wizara ya afya.

Majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Liith Mussawi na Ustadh Abbasi Rashidi Mussawi mkuu wa kitengo, pamoja na rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani na kundi la walimu na watumishi.

Mhadhara kuhusu masaaibu ya Ashura umetolewa na Shekh Abdullahi Dujaili, ameongea namna watu wa Imamu Hussein (a.s) walivyo jitolea na walivyo kuwa na ikhlasi ya kweli, hasa ndugu yake na mbeba pendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s), aliye tufundisha uaminifu, kujitolea na ushujaa, pamoja na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa ndugu yake.

Nae Sayyid Liith Mussawi akasema kuwa: “Kutokana na changamoto ya kuwepo kwa janga la Korona mwaka huu, kazi nyingi zimesimama kila kona ya dunia, lakini wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wameendelea kuomboleza msiba huu chini ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, ya kutekeleza maagizo ya idara ya afya na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Chuo kikuu cha Alkafeel kimekuwa mstari wa mbele daima katika kuhuisha matukio kama haya, yanayohusu shule ya kujitolea na uaminifu, ndio maana imefanya majlisi hii ya kuhuisha kifo cha Imamu Hussein (a.s) na kumpa pole Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wa nyumbani kwake (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: