Vituo vya Ashura: Rubabu aongea na kichwa kitakatifu cha Imamu Hussein (a.s).. hakika aliyekua nuru inayo angaza Karbala ameuwawa na hajazikwa

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa katika siku kama hizi mwaka (61) hijiriyya, baada ya mateka wa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupelekwa Kufa, Ubaidullahi bun Ziyadi aliamrishwa wawekwe kwenye nyumba mbovu iliyokuwa pembeni ya msikiti mkubwa, hakutosheka na aliyofanya kwa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake walipo fikishwa mbele yake, uovu wake ulimpelekea arudie kufanya mambo mabaya yanayochukiza kwa kila mtu, aliamrisha aletewe kwa mara nyingine kichwa cha Imamu Hussein (a.s), halafu akaagiza mateka waletwe mbele yake, wakaingia wakiwa wametanguliwa na bibi Zainabu (a.s), ibun Ziyadi akaanza kuchomachoma mdomo wa Imamu Hussein (a.s) kwa fimbo iliyokuwa mkononi mwake.

Walipo ingia kwake wakakuta kichwa cha Hussein (a.s) kipo mbele yake na kinatoa nuru ya Mwenyezi Mungu inayoangaza hadi mbinguni, Rubabu Mke wa Hussein (a.s) na mama wa Abdullahi na Sukaina (a.s) hakuweza kuvumilia, alisimama mbele ya watu, akakumbatia kichwa kile kitakatifu na kukiweka miguuni mwake, imekuja katika riwaya kuwa alipewa nafasi ya kuongea mbele ya ibun Ziyadi, akaongea kwa muhtasari wa ajabu, aliongea beti za mashairi zisemazo:

Hakika aliyekuwa nuru iangazayo Karbala, ameuwawa na muili wake haujazikwa.

Mjukuu wa Mtume, Mwenyezi Mungu akulipe mema na umeonyesha kipimo cha hasara.

Ulikuwa kwangu ni jabali madhubuti ninaekutegemea, ulikuwa ukituongoza kwa upole na kwa misingi ya Dini.

Mayatima ni wanani, na masikini ni wanani, nani atasimama na kutegemewa na kila masikini.

Wallahi sitafuti mkwe katika ukwe wenu hadi nitakapo toweka katika maji na udongo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: