Vituo vya Ashura: Mateka wa kizazi cha Mtume watoka Kufa kwenda Sham

Maoni katika picha
Msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) walipitia vituo na matatizo mengi, katika siku kama ya leo mwezi kumi na tisa Muharam mwaka (61) hijiriyya, msafara wa mateka hao ulitoka Kufa kwenda Sham ukiwa umetanguliwa na vichwa vya mashahidi, vilivyo tanguliwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s).

Baada wa watoto waliokulia katika wahyi, utume na uimamu kupata mateso ya aina tofauti walipo kuwa Kufa, walifungwa, wakanyanyaswa na kudhalilishwa kama watumwa, halafu ikatoka amri ya kupelekwa Damaska kwa Yazidi, ibun Ziyadi aliamrisha vichwa vya watoto wa Mtume (s.a.w.w) na wafuasi wao vipelekwa Sham na kutembezwa kwa watu wa huko kama vilivyo tembezwa kwa watu wa Kufa, ili kujaza hofu katika nyoyo za watu na kuonyesha uwezo wa bani Umayya.

Vichwa vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) vilipelekwa chini ya usimamizi wa Zuhairu bun Qais Aljuúfiy, na familia ya Mtume iliwekwa chini ya usimamizi wa Mahfar bun Thaálaba na Shimri bun Dhijaushan, walifungwa kamba na kupandishwa juu ya ngamia wasio kuwa na vitandiko vya kukalia wakasafiri katika mazingira magumu.

Mfasara wa mateka uliondoka Kufa kwenda Sham ukiwa umetanguliwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s) pamoja na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake walio uwawa na kukatwa vichwa vyao katika jangwa la Twafu, nyuma ya vichwa wakapangwa watoto na wanawake wakitanguliwa na bibi Zainabu (a.s) jemedari wa Karbala, akiwa pamoja na mtoto wa kaka yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s), aliyekuwa na minyororo mikononi mwake na kufungwa shingoni, walibebwa juu ya ngamia waliokuwa hawana tandiko za kukalia wala mwanvuli, walianza kukata masafa na kuelekea Damaska.

Tambua kuwa msafara wa Imamu Hussein (a.s) ulipitia hatua nyingi ikiwemo ile ya karibu na kifo chake (a.s), pamoja na hii ya baada ya kuuwawa kwake, ukiwemo msafara huu wa kupelekwa mateka wa nyumba ya Mtume (a.s) huko Sham.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: