Atabatu Abbasiyya tukufu inakabidhi jengo la Alhayaat la tano katika huko Bagdad kwa idara ya afya na imesisitiza kuwa kituo hicho kimekidhi vigezo vya kiujenzi na kiafya

Maoni katika picha
Asubuhi ya Alkhamisi mwezi (21 Muharam 1442h) sawa na tarehe (10 Septemba 2020m), Atabatu Abbasiyya imekabidhi jengo la Alhayaat la tano kwa idara ya afya katika mji mkuu wa Bagda kitongoji cha Raswafa, baada ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kilichopo katikaeneo la hospitali ya Ibun Qafu.

Hiki ni miongoni mwa vituo vikubwa vilivyo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na vinavyo jengwa kwenye mikoa tofauti, ujenzi huu ni sehemu ya kutekeleza maagizoya Marjaa Dini mkuu, aidha ni sehemu ya kusaidia wizara ya afya katika vita dhidi ya virusi vya Korona, kituo kinamejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (5000), kinavyumba vya wagonjwa (118) pamoja na vyumba (19) vya madaktari na wauguzi.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Mhandisi Samiir Abbasi amekabidhi fungua za jingo hilokwa makamo mkuu wa idara ya afya Dokta Hasanaini Mussawi, mbele ya mkuu wa hospitali ya ibun Qafu pamoja na jopo la wahudumu wa afya.

Mhandisi Samiir Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kituo kimejengwa ndani ya siku (55), kimegawanyika sehemu tatu: sehemu ya kwanza inaukubwa wa mita (1377) na inavyumba (56) pamoja na sehemu ya vyoo, vyumba hivyo vimegawika pange mbili, sehemu ya pili ni sawa na sehemu ya kwanza, ukubwa, mfumo wa ujenzi wake na idadi ya vyumba, sehemu ya tatu inaukubwa wa mita (1000), inavyumba (19) vya madaktari na wauguzi, imegawanyika sehemu mbili pia, vilevile kuna ukumbi wa kupokea wagonjwa wenye ukumbwa wa mita (100) na kuna sehemumbili za vyoo, upande mmoja wa wanaume na mwingine wa wanawake”.

Akaongeza kuwa: “Jengo linamifumo saidizi, kama vile mfumo wa kutoa tahadhari ambao umewekwa sehemu zote za jingo, mfumo wa umeme, mfumowa usambazaji wa waji, mfumo wa Kamera za ulinzi, mfumo wa viyoyozi kwenye vyumba vyote pamoja na mfumo wa kutoa hewa chafu na kuingiza safi (AIR FRESH) kwa kiwango kinacho endana na wagonjwa, hewa hutolewa nje baada ya kuitibu kwa mitambo maalum ili isilete madhara kwa watu”.

Makamo mkuu wa idara ya afya ameishukuru Atabatu Abbasiyya kwa msaada huu, amesema kuwa: “Atabatu Abbasiyya wakati wote imekuwa msaada mkubwa kwa raia wa Iraq, ipo mstari wa mbele katika kila jambo, ikiwa nipamoja na vita dhidi ya Korona, ambayo leo tumekuja kukabidhiwa jingo hili ambalo ni msaada mkubwa kwa sekta ya afya katika kupambana na janga la Korona, leo tumefanya makabidhiano baada ya kukamilisha taratibu zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kukagua sehemu zote za jingo na kujiridhisha kuwa zimekamilisha vigezo vyote vya afya, na jingo hili linaweza kutumika kama hospitali ya kawaida baada ya kuisha janga la Korona Insha-Allah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: