Marjaa Dini mkuu amesema kuwa: Uchaguzi ujao unatakiwa kuwa huru na wa haki bila kujali maslahi binafsi na vyama vya kisiasa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kuwa uchaguzi ujao unatakiwa kuwa huru, usioweka mbele maslahi ya watu binafsi na vyama vya siasa, pamoja na kutenda haki katika ngazi zote, usimamiwe na watu wenye uzowefu wakiwemo wajumbe wa umoja wa mataifa.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Hakika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwakani unaumuhimu mkubwa, inatakiwa ziundiwe kanuni zitakazo wezesha kuwa na uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwafanya wananchi washiriki kwa wingi, hivyo lazima ufanyike kwa misingi ya haki na uwadilifu bila kujali maslahi ya baadhi ya vikundi na vyama vya kisiasa, lazima haki izingatiwe katika ngazi zote, usimamiwe vizuri na watu waliobobea katika mambo ya uchaguzi wakiwemo wajumbe wa umoja wa mataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: