Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s), aliye pata shahada mwezi ishirini na tano Muharam, ndani ya ukumbi wa haram (mkabala na mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi a.s), chini ya kanuni zote za afya zilizo himizwa na Marjaa Dini mkuu pamoja na wizara ya afya.

Majlisi ya kuomboleza itafanyika siku mbili kuanzia jioni ya jana chini ya uhadhiri wa shekh Salami Askariy, na leo asubuhi mhadhiri alikua ni Sayyid Hisham Batwaat, kuna mhadhara mwingine wa jioni utatolewa na Sayyid Nasraat Qashaaqish Al-Aamiliy, na kuhudhuriwa na watumishi wa malalo takatifu na mazuwaru, kulingana na ukubwa wa sehemu sambamba na kujiepusha na msongamano.

Wazungumzaji wameeleza hatua alizopitia Imamu Sajjaad (a.s), ambapo hatua mbaya zaidi na inayo umiza sana ni tukio la Ashura na yaliyo mtokea baba yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, pamoja na kutekwa shangazi yake na dada zake na kuchukuliwa kutoka Karbala hadi Sham, kisha wakarudi Karbala hadi Madina (mji wa babu yake Mtume –s.a.w.w-), wakiwa katika mazingira magumu ambayo huzingatiwa kuwa ilikuwa hatua ya kukamilisha harakati ya baba yake (a.s), na namna walivyo kuwa yeye na shangazi yake Aqilatu Zainabu (a.s), jinsi walivyo fanikisha kuonyesha uovu na uongo wa bani Umayya, hali kadhalika wameongea kuhusu nafasi yake katika elimu na bila kuisahau Zaburi Aali Muhammad (Swahifatu Sajjaadiyya) pamoja na mambo mengine kuhusu mtu huyu mtakatifu.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jawaad Hasanawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu uendeshwaji wa majlisi hiyo, amesema: “Katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Sayyid Saajidina na pambo la waabudio Imamu Sajjaad (a.s), kama tunavyo fanya kila mwaka, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza msiba huo katika mazingira ya tofauti na miaka mingine, kutokana na kuwepo kwa janga la Korona ambalo limesababisha kuwepo kwa marufuku ya misongamano na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo cha utumishi kimechukua jukumu la kuandaa mahitaji yote ya majlisi hizo, ikiwemo kutandika ukumbi na kupanga viti kwa kuzingatia umbali unaokubalika kiafya, pamoja na kuweka vizuwizi, majlisi zitafanyika siku mbili, siku ya kwanza itakuwa na mhadhara wa jioni na miwili asubuhi na mwingine jioni ya siku ya pili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: