Katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi makubwa huku wakipiga vifua na kutokwa machozi, mawakibu za Karbala zimeomboleza kifo cha Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s), kama kawaida yao katika kuomboleza kifo cha Imamu Maasumu (a.s) jambo walilo rithishana kizazi baada ya kizazi, kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona mazingira ya uombolezaji wa mwaka huu yamekua tofauti na miaka mingine.
Makamo rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Hashim Mussawi amesema kuwa: “Asubuhi ya siku ya Jumatatu mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka sehemu tofauti za mji wa Karbala vilianza matembezi mapema asubuhi ya kuelekea kwenye malalo mbili takatifu, ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kutokana na msiba huu mkubwa uliotokea siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Muharam mwaka (94) hijiriyya”.
Akaongeza kuwa: “Kitengo chetu kimeandaa utaratibu wa kupokea mawakibu hizo na yeyote atakaekuja kuomboleza msiba huu, tayali zimesha pangwa njia watakazo tumia kuanzia mwanzo hadi mwisho, pamoja na kuzingatia masharti yote ya afya na kuyafanyia kazi, tumehakikisha hakuna msongamano na mawakibu zinatembea kwa urahisi, tumeweka watumishi wetu wanao ongoza matembezi ya mawakibu hizo kuanzia mwanzo hadi mwisho”.