Vituo vya Ashura: Makumbusho ya kituo cha Husseiniyya kusini ya Mosul

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa miji mingi ilipitiwa na msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) na vichwa vitakatifu, miji mingi imejenga makumbusho ya vituo vilivyo pitiwa na msafara huo, hakuna shaka kuwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s) hakikuzikwa katika vituo hivyo, lakini kiliwekwa au kuhifadhiwa katika maeneo hayo kwa wakati fulani, ikiwemo makumbusho ya Mosul, nao ni mji uliopo kaskazini ya Iraq pembezoni ya mto Dujla, umbali wa kilometa (600) kutoka mji wa Kufa, katika mji huo kuna makumbusho iitwayo (makumbusho ya tone la damu ya kichwa cha Hussein) hadi karne ya saba hijiriyyah/ sawa na karne ya kumi na tatu miladiyya, sehemu ambayo kiliwekwa kichwa cha Imamu Hussein wakati msafara wa mateka ulipo pita eneo hilo ilikua inatoa damu” kama ilivyo pokewa katika kitabu cha (Ishaaraat).

Katika kitabu cha (Nafsi Mahmuumu) kimeandika kuwa: Kuhusu makumbusho ya Mosul “Msafara ulipotaka kuingia Mosul alitumwa mfanyakazi aende akawaambie waandae zawadi na kupamba mji, watu wa Mosul wakakubaliana kutowaingiza katika mji huo, bali wapiti nje ya mji.

Wakasimama nje ya mji umbali wa farsakh (kilometa tano takriban) na wakaweka kichwa juu ya jiwe, damu ya kichwa kitakatifu ikadondokea kwenye jiwe hilo, jiwe likawa linatoka damu kila mwaka katika siku ya Ashura, watu walikuwa wanakusanyika kwenye jiwe hilo na kuomboleza kila siku ya Ashura, hali hiyo iliendelea hadi wakati wa utawala wa Abdulmalik bun Marwani, akaamuru kutolewa jiwe hilo, kuanzia hapo haikuonekana tena athari ya damu, lakini sehemu hiyo palijengwa kubba na wakaliita (Mash-hadu-Niqtwa)”.

Katika kitabu cha (Alkaamil) cha Bahaaiy kimeandika kuwa: Wabebaji wa kichwa kitakatifu walikuwa wanaogopa makabila ya waarabu yasije kuwanyangánya kichwa hicho, wakaacha kupita njia inayo julikana, kila walipo fika katika kabila fulani waliomba urafiki na kuwaambia tunakichwa cha Khaarijiy.

Shekh Auhadi ametunga shairi kuhusu kurudi kwa uombolezaji kila mwaka kwa kifarisi na kutafsiriwa kwa kiarabu lisemalo:

Kila mwaka tunahuzunika upya *** huzuni isiyo isha na machozi yetu hayakauki.

Sehemu nyingine imetajwa kuwa –kuhusu sababu za kujengwa makumbusho hiyo- baada ya kuuwawa Imamu Hussein (a.s), walibeba kichwa chake hadi Sham, wakapita katika mji wa Dairu-Saidi, wakalala karibu na mji huo, huku kichwa cha Hussein (a.s) kikiwa kimechakaa, mmoja wa makasisi wa Dairu akakiomba, akakichukua na kukiosha halafu akakipata marashi, akalala nacho usiku mmoja, likadongoka tone la damu kutoka kwenye kichwa hicho pale katika ardhi kilipo lala, kasisi huyo akajenga makumbusho sehemu hiyo, na kuitwa makumbusho ya tone la damu ya Husseiniyya, na sehemu hiyo ikafanywa ya kuzikia watu mashuhuri wa Mosul.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: