Kongamano la kitamaduni la Ashura litafanywa kwa njia ya mtandao na kutakuwa na mashindano pamoja na zawadi kwa washindi

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuwa itafanya kongamano la kitamaduni la Ashura awamu ya nane mwaka huu kwa njia ya mtandao, kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Bagdad kutokana na kuwepo kwa janga la Korona na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya, siku ya Ijumaa ijayo tarehe (18 Septemba 2020m) saa kumi na moja jioni.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Maahir Khalidi kiongozi wa idara hiyo: “Kongamano ni moja ya harakati muhimu za Idara, lilipata muitikio mkubwa katika awamu zilizo pita, ili kuhakikisha mawasiliano yanaendelea kamati imeamua kuendesha kongamano hilo kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (ZOOM) chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, wito wa kushiriki kwenye kongamano hilo umetolewa ndani na nje ya chuo, tunatarajia kufanikisha malengo ya kongamano, ya kumbukumbu na malengo yake matukufu kupitia vipengele tofauti”.

Akafafanua kuwa: “Miongoni mwa ratiba ya kongamano hilo kuna shindano la kitamaduni, milango ya kushiriki kwenye shindano hilo imefunguliwa kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/cont na tutapokea majibu yao ndani ya kipindi hiki, majina ya washindi yatatangazwa mwishoni mwa ratiba ya kongamano pamoja na kutoa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, baada ya kupitia majibu yao na kupiga kura kama kukiwa na washindi wengi ili kuwapata washindi watatu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: