Kituo cha turathi za Karbala kimetangaza kufanyika kongamano la kielimu na kimataifa la kwanza

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanya kongamano la kwanza kwa njia ya mtandao kuhusu turathi za Karbala kupitia jukwaa la (zoom) chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ni utambulisho wetu), siku ya Jumamosi mwezi (6 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (24 Oktoba 2020m).

Kongamano litakuwa na mihadhara miwili (asubuhi na jioni) link ya kujiunga na kongamano kwa (zoom) itatangazwa hivi karibuni.

Mkuu wa kituo cha turathi za Karbala Dokta Ihsani Gharifi amesema kuwa: “Kwa sababu ya kuwepo maambukizi ya virusi vya Korona duniani, na ulazima wa kuheshimu maelekezo ya idara ya afya, ikiwepo kujiepusha na misongamano, pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, na kushindikana kufanyika makongamano mengi ya kimataifa, kutokana na ugumu wa kusafiri nchi moja hadi nyingine na kufungwa viwanja vya ndege na ugumu wa kupata viza, pamoja na kuogopa kusambaza maambukizi ya virusi vya Korona kwenye mikusanyiko ya watu, kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeamua kufanya kongamano la kielimu na kimataifa liitwalo (Turathi za Karbala na nafasi yake katika maktaba za kiislamu) kwa njia ya mtandao”.

Akaongeza kuwa: “Kongamano litafanyika kupitia jukwaa la Zoom chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ni utambulisho wetu) siku ya Jumamosi mwezi sita Rabiul-Awwal 1442h, sawa na tarehe (24 Oktoba 2020m) na litaendelea hadi siku ya Jumapili kutokana na idadi ya watoa mada watakao shiriki”.

Akaendelea kusema: “Jumla ya mada za kitafiti zilizo omba kushiriki hadi sasa zimefika (192) kutoka nchi tofauti duniani, kama vile Uingereza, Ujerumani, Marekani, Misri, Sirya, Lebanon, Iran, Baharain na zinginezo, pamoja na watafiti kutoka vyuo tofauti vya Iraq”.

Akasema: “Kongamano litakuwa na vikao viwili kwa siku, kikao cha asubuhi na jioni, washiriki watapewa vyeti vya ushiriki, na wale watakao hudhuria pia watapewa vyetu vya uhudhuriaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: