Vituo vya Ashura: Naswibiyiin ilihifadhi kichwa kitakatifu cha Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa historia wanasema kuwa msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) ulipita katika miji mingi, na maeneo mengi yamejenga makumbusho sehemu ambazo msafara huo ulipita, bila shaka kichwa cha Imamu Hussein (a.s) hakikuzikwa katika maeneo hayo, lakini kiliwekwa au kuhifadhiwa sehemu hizo kwa muda, miongoni mwa sehmu hizo ni Maqaam Ra-asu Sharifu katika mji wa Naswibiyiin.

Naswibiyiin kwa fat-ha kisha kisra kisha yee ya alama ya Jam’u swahihi, ni mji uliopo katika maeneo ya Jazira kati ya Mosul na Sham, kuna bustani elfu Arubaini, kati yake na Sanjaar kuna farsakh tisa, kutoka hapo hadi Mosul ni mwendo wa siku sita, eneo hilo kwa sasa lipo Uturuki kwenye mpaka wake na Sirya, na unatenganisha na mji wa (Qamishliy) Sirya mstari wa mpaka.

Imepokewa katika baadhi ya vitabu kuwa msafara wa mateka ulipofika Naswibiyiin, kiongozi wa mji huo aliamuru upambwe, wakaweza zaidi ya mapambo laki moja, na wakapandisha zaidi ya pendera elfu moja za kupokea kichwa cha Imamu Hussein (a.s), Mal-uuni aliyekuwa amebeba kichwa cha Imamu Hussein (a.s) akataka kuingia katika mji huo, farasi wake hakumtii, akabadili farasi mara kadhaa na zote hazikumtii, mwisho kichwa kitakatifu kikadondoka kutoka juu yamkiki, waliokuwepo eneo hilo wakatambua kuwa ni kichwa cha Imamu Hussein (a.s), wakawalaumu na kuwakemea kisha kichwa kile wakakiweka nje ya mji, na wala hawakuingia nacho katika mji… Shekh Abbasi Qummiy anasema: Sehemu kilipoanguka kichwa hicho kitakatifu ndio palipojengwa makumbusho.

Mji huo unamakumbusho tatu:

  • - Masjid Imamu Zainul-Aabidina (a.s).
  • - Mash-hadu Ra-asi katika moja ya masoko yake, sehemu kilipo wekwa kichwa kitakatifu wakati msafara wa mateka unapita.
  • - Mash-hadu Nuqtwa, inasemekana lilidondoka tone la damu ya kichwa cha Imamu Hussein (a.s) sehemu hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: