Watumishi wa kikosi cha Abbasi wanapuliza dawa katika mkoa wa Waasit

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wameanza kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Waasit kwenye maeneo yatakayo tumiwa na mawakibu pamoja na kufanyiwa majaalisi Husseiniyya, tayali wamesha puliza sehemu nyingi zitakazo tumika kufanyia Majaalisi hizo tukufu.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Tuliunda kikosi maalum kwa ajili ya kazi hiyo toka mwanzoni mwa mwezi wa Muharam, na kimekuwa kikifanya kazi kila siku katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Waasit, aidha kikosi hicho hupuliza dawa pia katika nyumba zenye watu walioambukizwa virusi vya Korona, pamoja na kwenye majengo na taasisi za serikali.

Wakazi wa mkoa wa Waasit na wahudumu wa mawakibu na majaalisi Husseiniyya wametoa shukrasi nyingi kwa kazi kubwa inayo fanywa na kikosi hicho, ya kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda jopo maalum la kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona tangu siku za kwanza kuripotiwa janga hilo, na kimekuwa kikipuliza dawa sehemu mbalimbali hususan kwenye makazi ya watu, na kinafanya kila kiwezalo katika kupambana na janga hili ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kuosha, kuvisha sanda na kuzika watu waliokufa kwa janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: