Vituo vya Ashura: Masjid ya Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Hama

Maoni katika picha
Msafara wa mateka ambao ni watoto na watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s), ni sawa na sehemu ya pili ya harakati ya Husseiniyya ya milele, bila msafara huo juhudi na shahada ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake ingepotea na isingejulikana, hatua hii ilianza baada ya kuuwawa kwake kishahidi (a.s), pale Ibun Saadi alipo ondoka na familia ya Hussein (a.s), akabeba wanawake wa nyumba ya Mtume kwenye ngamia wasiokuwa na vitandiko vya kukalia, aliwabeba kama wanavyo bebwa mateka wa kituruki na kirumi, kutoka Karbala hadi Kufa kisha kutoka Kufa hadi Sham.

Watu wa historia wanasema kuwa msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) ulipita katika miji mingi, na maeneo mengi yamejenga makumbusho sehemu ambazo msafara huo ulipita, bila shaka kichwa cha Imamu Hussein (a.s) hakikuzikwa katika maeneo hayo, lakini kiliwekwa au kuhifadhiwa sehemu hizo kwa muda, miongoni mwa sehemu hizo ni mji wa Hama.

Hama, ni mji uliopo katika eneo la Homsi, umezungushiwa uzio wa mawe, na kunajengo kubwa la mawe, kuna mto A’aswi unapita mbele yake na kumwagilia bustani zake nao ni mji wa zamani, ametaja Iru-u Qais katika shairi lake na baadhi ya wanachuoni wamenukuu kutoka kwa Arbabu Maqaatil kuwa: alipita katika njia ya Hama akaona msikiti uitwao Masjid Hussein (a.s) kwenye bustani zake, akaingia ndani ya msikiti huo akakuta pazia imewekwa ukutani, anasema: nikaondoa pazia nikaona jiwe limewekwa ukutani likiwa na athari ya alama ya shingo na kichwa pamoja na damu iliyo kauka, nikauliza watumishi wa msikiti: hili jiwe la nini na kwa nini lina athari ya damu? Nikaambiwa: Jiwe hili kiliwekwa kichwa cha Hussein (a.s) juu yake na watu waliokuwa wamekibeba wakati wanakwenda Damaskas ndio athari hiyo ikabaki kwenye jiwe kama unavyo ona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: