Hivi punde.. Ofisi ya Sayyid Sistani imetangaza kuwa kesho siku ya Jumamosi ni mwezi mosi Safar

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, Ayatullah Sayyid Ali Sistani imetangaza kuwa, kesho siku ya Jumamosi tarehe (19 Septemba 2020m) ni siku ya kwanza ya mwezi wa Safar mwaka (1442h).

Hivyo tarehe nane mwezi wa kumi itakuwa ndio siku ya mwezi (20) Safar siku ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Safar ni mwezi wa pili katika mwaka wa mwezi au hijiriyya baada ya mwezi wa Muharam, mwezi ishirini Safar wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) hufanya maombolezo ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), mamilioni ya watu humiminika katika mji wa Karbala wakitembea kwa miguu kwa ajili ya maombolezo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: