Dondoo za kumbukumbu: mwezi pili Safar aliuwawa kishahidi jemedari Zaidu bun Ali (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi pili Safar mwaka wa (122h) aliuwawa kishahidi mpambanaji Abu Hussein Zaidu Shahidi bun Imamu Ali Sajjaad bun Imamu Abu Abdillahi Hussein bun Amirulmu-Uminina Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Tuangazie kisa cha kifo chake kupitia historia iliyo andikwa na marehemu Sayyid Muhsin Amiin Al-Aamiliy katika kitabu chake kiitwacho (Majaalisu Suniyya), anasema: Zaidu bun Ali bun Hussein (a.s) alikuwa tegemeo la ndugu zake baada ya kaka yake Abu Jafari Baaqir (a.s) na alikuwa mbora wao, alikuwa mchamungu, mnyenyekevu, faqihi, shujaa, alishika siraha kupigana, aliamrisha mema na kukataza maovu, alipigana kulipiza kisasi cha Hussein (a.s), miongoni mwa sababu za kupigana kwake ilikuwa na kutetea damu ya Hussein (a.s), aliingia kwa Hisham bun Abdulmalik huku Hisham akiwa amekusanya watu wa Sham, akawaamrisha wamzuwie asifike karibu yake.

Zaidu akamuambia hakika hakuna mja yeyote wa Mwenyezi Mungu anayeusia kumcha Mwenyezi Mungu, na mimi nahusia kumcha Mwenyezi Mungu na ninakutaka umche Mwenyezi Mungu.

Hisham akasema: Kitugani amefanya ndugu yako Baqarah (ng’ombe)?

Akasema: Mtume (s.a.w.w) alimwita Baaqirul-Ilmu, na wewe unamwita Baqarah (Ng’ombe)! Kwa sababu ya tofauti zenu za duniani na hakika mtatofautiana akhera!

Hisham akasema: unatarajia kuwa khalifa? Uko mbali sana wewe na ukhalifa, hauna mama, hakika wewe ni mtoto wa mama.

Zaidu akamuambia: Mimi sijui mtu mwenye daraja kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda Mtume ambaye ni mtoto wa mama, ingekuwa hilo linapunguza utukufu wa mtu asingefanywa kuwa Mtume, naye ni Ismail bun Ibrahim (a.s), utume unadaraja kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu au ukhalifa ewe Hisham? Nini kasoro ya mtu ambae baba yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), naye ni mtoto wa Ali bun Abu Twalib (a.s).

Hisham akasimama na akaagiza walinzi wake wamzuwie, akasema: Huyu msimuache katika jeshi letu.

Zaidu akatoka huku anasema: Hakika watu hawatachukia upanga katu ispokuwa watadhalilika, hisham akapelekewa neno hilo, akatambua kuwa anakwenda kujiandaa aje kupigana nae, akamtumia askari wa kumpeleka hadi kwenye njia ya Hijazi na wala wasimruhusu aende njia ya Iraq, wakampeleka hadi kwenye njia ya Hijazi halafu wakarudi. Na yeye akarudi Iraq akaenda katika mji wa Kufa, watu wakaanza kukusanyika kwake na kula kiapo cha utii, wakazi wa Kufa waliomuunga mkono wakafika elfu kumi na tano, ukitoa watu wa Madaainu, Basra, Waasit, Mosul, Khurasani, Ray, Jarjaan na Jazira. Wakapambana na jeshi lililokuwa likiongozwa na Yusufu bun Amru Thaqafiy, walipo ingia vitani jeshi la Zaidu likashindwa, akabaki na watu wachache, akapigana vita kali sana huku anasema:

Maisha ya udhalili na kifo cha utukufu vyote naviona sawa na chakula.

Ikiwa lazima nichague kimoja takimbilia kifo kwa furaha.

Usiku ukaingia akiwa Swifiin, Zaidu akaondoka akiwa na majeraha makubwa, alikuwa amepigwa mkuki kwenye paji la uso wake, akatafuta mtu wa kumtoa mkuki akaenda kwa daktari, akamtoa mkuki huo na akafa wakati huohuo, akazikwa kwenye njia ya maji na wakaweka juu ya kaburi lake udongo na majani kisha wakafungulia mali yapite juu ya kaburi lake, daktari akahudhuria mazishi hayo na akawa amefahamu sehemu alipo zikwa, palipo pambazuka akaenda kwa Yusufu akamuonyesha sehemu lilipo kaburi, Yusufu akaenda kufukua kaburi na kutoa muili wake halafu akakata kichwa na kukipeleka kwa Hisham. Hisham akakipeleka kichwa hicho Madina na kukiweka juu ya kaburi la Mtume (s.a.w.w) mchana na usiku.

Taarifa za kuuwawa kwake zikamfikia Swadiq (a.s) alihuzunika sana kwa msiba huo, akagawa mali kwa familia za watu waliouwawa pamoja nae dinari elfu moja, Hisham akamuandikia Yusufu bun Amru kuwa ausulubu muili ukiwa bila nguo, akausulubu muili ukiwa mtupu, buibui akazungusha uzi wake sehemu ya utupu, muili ulisulubiwa miaka minne, hadi alipo kufa Hisham na akatawala Walidi bun Yazidi, Walid akamuandikia Yusufu bun Amru: Ammaa ba’ad, utakapo pata barua yangu fanya haraka kwenda Iraq na uchome muili wa Zaidu kisha jivu lake ulirushe hewani.

Kwa hakika Zaidu aliuwawa kifo kibaya mmno, kinacho umiza kila mtu mwenye ubinaadamu, hakuna hila wala nguvu ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu mkuu, watatambua walio dhulumu wapi watakapo fikia na mwisho mwema ni wa wachamungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: