Kwa ukubwa wa vitanda (100): Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua jenge la Alhayaat la saba katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatatu mwezi (3 Safar 1442h) sawa na tarehe (21 Septemba 2020m), imezindua jengo la Alhayaat la saba katika mkoa wa Baabil, katika eneo la mji wa Marjani kitabibu, baada ya kukamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi na kwa ubora mkubwa unao endana na sababu za ujenzi wa kituo hicho, chini ya watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Ataba tukufu, kituo kimejengwa ndani ya siku (54) tu, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) na kinavitanda vya wagonjwa (100) na jumla ya vyumba (98), aidha kuna vyumba vingine vya madaktari, wauguzi na wahudumu wengine vipatavyo (25), jengo kwa sasa lipo tayali kutoa huduma.

Hafla ya uzinduzi imefanyika kwenye uwanja wa mbele ya jengo hilo na imehudhuriwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu pamoja na wawakilishi wa serikali na idara ya afya, bila kumsahau daktari mkuu wa Marjana na viongozi wengine.

Baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi kulikuwa na ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na makamo katibu mkuu Mhandisi Abbasi Mussawi, amesema kuwa: Ataba takatifu inaendelea kusaidia wahudumu wa afya kupambana na janga la Korona, ujenzi wa vituo vya Alhayaat ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo mchango wetu katika vita hiyo, pamoja na mazingira magumu tuliyo nayo hayaja zuwia kufanya ujenzi huu, kituo hiki ni sehemu ya majengo saba yaliyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo yamekamilisha sifa na vigezo vya kiafya..

Ukafuata ujumbe wa serikali ya eneo hilo ulio wasilishwa na msaidizi wa kitaalam wa mkuu wa mkoa wa Baabil Mhandisi Hamidi Ali Zarkani, ambae ametoa shukrani za serikali ya mkoa kwa Atabatu Abbasiyya na watumishi wake wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha saba kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kituo ambacho ni msaada mkubwa katika kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa na kusaidia wahudumu wa afya kupambana na janga la Korona..

Ukafuata ujumbe wa idara ya afya ya mkoa ulio wasilishwa na mkuu wa idara hiyo Dokta Muhammad Hashim Jafari, akabainisha kuwa jengo la Alhayaat la saba limejengwa na Atabatu Abbasiyya hapa mkoani katika mazingira haya magumu ambayo taifa linapitia kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ni fahari kubwa na litaendelea kuwa kielelezo kinacho onyesha mchango wa Ataba tukufu katika vita dhidi ya janga hili, jengo hili ni msaada mkubwa katika sekta ya afya hapa mkoani kwetu.

Zikafuata pongezi na shukrani kutoka kwa viongozi mbalimbali, walio shukuru Atabatu Abbasiyya na watumishi wake waliofanikisha ujenzi wa mradi huu.

Kisha watu wote wakaelekea kwenye uzinduzi wa jengo na kulitangaza rasmi kuwa limeanza kutoa huduma, baada ya kusikiliza maelezo kwa ufupi kutoka kwa watekelezaji wa mradi huo walio eleza huduma zinazo patikana katika jengo hilo.

Kumbuka kuwa ujenzi huo umefanywa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) kuna jumla ya vyumba vya wagonjwa (98) na zaidi ya vyumba (25) vya madaktari, wauguzi na watumishi wengine, ni moja ya majengo saba yaliyojengwa katika mikoa tofauti, kama vile, Bagdad, Muthanna, majengo mawili katika mji wa Hussein (a.s) wa kitabibu na moja katika hospitali kuu ya Hindiyya mkoani Karbala, ujenzi huo ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu na chini ya muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ya kusaidia sekta ya afya katika kupambana na janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: