Maelekezo ya kiafya kwa mawakibu za uombolezaji na za kutoa huduma zinazo shiriki katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imetoa maelekezo ya kiafya kwa mawakibu za kuomboleza na za kutoa huduma zinazo shiriki katika ziara ya Arubaini na kuhimiza ulazima wa kuheshimu maelekezo hayo, yanaendana na maelekezo ya idara ya afya ili kuhakikisha usalama wa kila mtu katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona, na kulinda afya za mazuwaru na waombolezaji.

Mambo yaliyo elekezwa ni:

  1. Lazima kuvaa soksi za mikononi wakati wa kufanya kazi kwenye maukibu na wakati wa kwenda kwenye majlisi za kuomboleza.
  2. Lazima kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono muda wote pamoja na kupuliza dawa kwenye eneo la maukibu na husseiniyya.
  3. Kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu wakati wa matembezi ya maukibu za waombolezaji na kwenye majlisi kama ilivyo elekezwa na idara ya afya.
  4. Upikaji wa chakula ufanywe ndani ya husseiniyya katika sehemu zilizo tengwa kwa ajili ya upishi ambazo zimekamilisha masharti ya afya.
  5. Ugawaji wa chakula na vinywaji kwa mazuwaru ufanywe kwa kutumia vifungashio (tak away) na vyombo vyenye mifuniko.
  6. Maukibu zitembee katika njia zilizo pangiwa.
  7. Kuandaa sehemu ya dharura ya kutolea huduma ya afya katika kila maukibu au kikundi, na kila maukibu iwe na watu (2-3) wenye jukumu la kuhimiza kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono pamoja na kupuliza dawa na kutekeleza masharti yote ya idara ya afya.
  8. Inapasa kumzuwia mtu yeyote kushiriki kwenye maombolezo au majlisi ya Husseiniyya kama hajavaa soksi za mikononi na barakoa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: