Baina ya haram mbili tukufu imewekwa mistari ya waombolezaji wanao omba kutatuliwa shida zao kwa utukufu wa bibi Ruqayyah (a.s)

Maoni katika picha
Katika tukio la kila mwaka la kuomboleza kifo cha kipenzi wa Imamu Hussein (a.s) aliyekufa siku kama ya kesho, na kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.

Jioni ya leo mwezi (4 Safar 1442h) sawa na tarehe (22 Septemba 2020m) imefanywa shuguli maalum ya kuomboleza, imeshuhudiwa mistari mirefu ya waombolezaji, na shughuli hiyo kupewa jina la bibi Ruqayyah (a.s) aliyefariki kwa huzuni huko Sham, akiwa amekumbatia kichwa cha baba yake Imamu Hussein (a.s) siku ya mwezi tano Safar 61h.

Maombolezo hayo ambayo yamefanywa kwa mwaka wa saba mfululizo yamefunguliwa na umoja wa kimataifa wa watumishi wa bibi Ruqayyah (a.s), na kwa kushirikiana na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni kawaida ya watu wa Karbala kufanya maombolezo haya pamoja na mazuwaru wa malalo mbili takatifu, wamefungua kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Sayyid Hashim Batwaat na kaswida za kimashairi yalio amsha hisia za huzuni wa msiba huo mkubwa, pia ilionyeshwa tamthiliya iliyo ongeza machungu na majonzi ya kifo cha bibi Ruqayyah (a.s).

Kuhusu mstari ulio wekwa; ni busati la kijani lililowekwa vipande vya miba kama ishara ya kukumbuka shahidi huyo alivyo tembea juu ya miba siku ya mwezi kumi Muharam (Ashura), pamoja na kandili na mishumaa pembezoni mwa mistari hiyo, waombolezaji wamekusanyika pembezoni mwa mistari hio na kuomba shida zao hususan wanawake na watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: