Kitengo cha kulinda nidham: Tumekamilisha maandalizi yote ya kupokea mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha kulinda nidham chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa lengo la kulinda usalama wa mazuwaru jambo ambalo linapewa umuhimu na Ataba tukufu, kwa kuwasiliana na idara husika kama vile askari wa Karbala na Atabatu Husseiniyya sambamba na kupangilia matembezi kwa utaratibu mziri.

Makamo rais wa kitengo cha kulinda nidham bwana Ahmadi Shaakir Mussawi amesema kuwa: “Kitengo cha kulinda nidham kina mikakati maalum kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara ya Arubaini, mwaka huu tumeandaa mkakati unaoendana na mazingira yaliyopo ya janga la Korona, tumeandaa barakoa, soksi za mikononi na vitakasa mikono kwa ajili ya watoa huduma walio ajiriwa na wanaojitolea, ili waweze kutumia wakati wa kutekeleza wajibu wao na kuwasaidia mazuwaru pia”.

Akaongeza kuwa: “Mwaka huu tunawatu wa kujitolea (2000) kutoka vikundi tofauti na mawakibu Husseiniyya zilizo zowea kujitolea kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watashirikiana nasi katika kutekeleza majukumu hayo”.

Akasema: “Kazi zimegawanyika sehemu tatu: amani, afya na huduma, amani inahusika na ukaguzi na ulinzi, kwa kutumia mitambo ya kisasa katika kufanya ukaguzi na ulinzi ndani na nje, afya inahusika na kuwapuliza dawa mazuwaru wanao ingia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuwahimiza kuvaa barakoa na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu, huduma ni pamoja na kuongoza matembezi ya mawakibu za waombolezaji wakati wa kuingia na kutoka ndani ya Ataba tukufu”.

Tambua kuwa kitengo cha kulinda nidham ni sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kila kiwezalo katika kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s) katika ziara zote kubwa ikiwemo hii ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: