Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kimemaliza kupuliza dawa kwenye vituo vya mitihani mkoani Basra

Maoni katika picha
Wahudumu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wamemaliza kazi ya kupuliza dawa katika vituo vya mitihani mkoani Basra.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: opresheni hiyo imehusisha Maahadi ya teknik na chuo cha teknolojia cha kusini mwa Basra, kutokana na ufanyaji wa mitihani ya darasa la sita iliyofanyiwa kwenye vituo hivyo.

Akaongeza: kazi hii imefanywa kwa kushirikiana na kamati ya kupambana na maambukizi ya mkoani hapa pamoja na wataalam wengine na imedumu kwa muda wa siku 23.

Wajumbe wa kamati ya kupambana na maambukizi wametoa shukrani nyingi kwa wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kazi kubwa waliyo fanya ya kuhakikisha mitihani inafanywa kwenye mazingira salama baada ya kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona siku zote za mitihani.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona mara tu baada ya kugudulika janga hilo, kamati hiyo imekua ikipuliza dawa kwenye maeneo mbalimbali hususan sehemu za makazi ya watu, na inafanya kila iwezalo katika kutekeleza swala hilo, aidha imejenga kituo cha kuosha, kuvisha sanda na kuzika watu waliokufa kwa janga la Korona mkoani Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: